Genesis 10

Mataifa Yaliyotokana Na Nuhu

(1 Nyakati 1:5-23)

1 aHawa ndio wazao wa Nuhu: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

Wazao Wa Yafethi


2 bWana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

3 cWana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

4 dWana wa Yavani walikuwa:
Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

Wazao Wa Hamu


6 eWana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misri,
Yaani Misri .
Putu na Kanaani.

7 gWana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.

8 hKushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. 9 iAlikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” 10 jVituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 11 kKutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, 12na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.


13 Misri alikuwa baba wa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
14 lWapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.

15 mKanaani alikuwa baba wa:
Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,
16 nWayebusi, Waamori, Wagirgashi,
17 oWahivi, Waariki, Wasini,
18 pWaarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,
19 qna mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

Wazao Wa Shemu

21 rShemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.


22 sWana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

23 tWana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

24 uArfaksadi alikuwa baba wa Shela,
naye Shela akamzaa Eberi.

25 Eberi akapata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

26 Yoktani alikuwa baba wa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
27 vHadoramu, Uzali, Dikla,
28 wObali, Abimaeli, Sheba,
29 xOfiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

30Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

32Hizi ndizo koo za wana wa Nuhu, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.
Copyright information for SwhKC